ImgWonders
  1. Homepage
  2. storynzuriiplanet_com

#storynzuriiplanet_com hashtag

Posts attached with hashtag: #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Kigamboni Bridge

Riwaya: MSITU WA SIRI 17 Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA Nlianza kuingiwa na amani na nikapata matumaini ya kurudi salama nyumbani....mara kwambali naona watu wakikimbia ovyo kila mtu alipita njia yake......nilipotizama vizuri niliona kiumbe kile kimeingia kijijini kwetu... ****Endelea*** niliona wanakijiji wakikimbiahuku na huku kila mmoja alipita njia yake....niliingiwa na wasiwasi kuwa mama yanguatakuwa hatarini... nilitimua mbio kuelekea nyumbani..wakati nakimnia watu walinishanhaa..na kuniona kuwa nimechanganyiki wa...kwanini nikimbilie kule kwenye hatari wakati wao wanakimbia kwaajili ya kwenda kujificha ili waokoe usalama wa maisha yao"",, nilikimbia nikaingia mpaka ndani huku naita MAMA MAMA..... nilipotazama vizuri sikumuona mama nikaamua kutoka nje... nilisikitika sana kuona maiti nyingi za wanakijiji zikiwa zimetapakaa chini kama mchanga"" nilizitazama maiti zile ili niangalie kama miongoni mwa maiti zile huenda nikamuona mama yangu"" nilitazama maiti moja hadi nyingine kwa umakini zaidi...ndipo nikagundua kuwa hienda mama yangu bado Yuhai.....nikakimbia nisijue naelekea wapi....mara kwa mbali nilimuona mama nilifurahi sana nikaita mama kwa kupaza sauti lakini mama hakunisikia kutokana alichanganyikiwa juu ya kiumbe huyu wa ajabu kwa kuuwa watu... ****** nilipoona haisikii sauti yangu nikaamua kukimbia kuelekea ule upande aliokuwa mama...mara ghafla nilimuona kiumbe yule akimfuata mama alikuwa nyuma kama hatua kumi hivi...niliogopa sana...nikapaza sauti tena nikaita mama..mama..ghafla kiumbe kile kikaacha kumfaya mama kikasimama..kikageuza shingo kutazama ule upande niliopo...kiumbe yule alinitazama kisha akaendelea kumfuata mama...nilimuonea huruma mama yangu alikuwa anakimbia huku kanga zikimdondoka.... nikatoa mshale nikauweka kwenye upinde nikauvuta kwa nguvu zangu zote huku nikikumbuka mjomba paul alipokuwa akinifundisha jinsi ya kulenga kitu kikiwa mbali bila kukikosa...nilivuta kisha nikaachia mshale ule""" ulienda moja kwa moja mpaka kwenye mgongo wa kiumbe yule... #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Dar es Salaam, Tanzania

Simulizi: MSITU WA SIRI 01 Mtunzi: YOZZ PIANO MAYA Baada ya baba yake DAVID kufariki..yapata miezi kumi sasa""" Nyumba yao ilipigwa mnada baada ya mama David kushindwa kulipia deni alilokopa BENKI marehemu mume wake....baada ya nyumba hiyo kupigwa mnada mama David aliamua kwenda kuishi kwenye nyumba ya kupanga,, wakati huo DAVID alikuwa anaumri upoatao miaka mitano",,baada ya kukaa miaka kadhaa alishidwa kumudu kulipia kodi ya nyumba kutokana na kipato chake kuwa kidogo""hivyo hakikuweza kutosheleza kulipia kodi ya nyumba na kutosha mahitaji mengine ikiwemo ada ya kumsomesha David. hivyo mama DAVID alilazimika kurudi kijijini kutokana na ugumu wa maisha huko mjini" ndipo alipoamua kuuza kila kitu cha ndani kwa lengo la kujipatia pesa ambayo itamsaidia kujikimu huko kijijini. ******* alifanikiwa kuuza vitu hivyo, alipata pesa zipatazo milioni mbili na laki tatu,, walifunga safari kutoka dar es salaam kuelekea igunga mkoani Tabora, mama david alionekana kuwa mnyonge na uso wake ulionekana ni mtu mwenye huzuni,, alikuwa akifikiria sana jinsi ya kwenda kuanzisha maisha mapya tena ya kijijini'' roho ilimuuma sana kutokana alikuwa ameshayazoea maisha ya mjini..pia alimkumbuka marehemu mume wake ambaye ndiye baba wa mtoto wake huyo wa kiume aitwae david,, alikumbuka vitu vingi alivyovifanya na baba David enzi za uhai wake... machozi yalimtoka....David alimuangalia mama yake kwa huruma,, ndipo David aliamua kumfuta machozi mama yake" mama Daivid alishindwa kujizuia alimtazama mwanae kisha akalia kwa uchungu huku amemkumbatia David...wakati huo David hakuelewa kitu chochote kutokana na umli wake kuwa mdogo..aliona kawaida kwa sababu alizoea kumuona mama yake akilia kila siku" dereva wa basi hilo aliliwasha gari na safari ya kuelekea Igunga ikaanza,, ****** watu (abiria) waliokuwemo ndani ya basi hilo walimtazama kwa nyuso za mshangao mama David kwa sababu alikuwa bado analia..wengiwao walihisi labda kapatwa na msiba hivyo zilisikika sauti za watu tofauti tofauti zikimwambia pole.. mama Davidi alijikaza na kuacha kuendelea kulia. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Dar es Salaam, Tanzania

SIMULIZI = DEBORA 02 maisha yalianza kusonga huku Debora akianza vimbwanga vyake kila kukicha, kwakuwa yeye ndo alikuwa akileta asilimia themanini na tano ya mahitaji yote ya ndani 85% hivyo ilimpa kiburi ya kutamba na kujiona yeye ndo yeye,, Ilikuwa ni mwiko kwa ndugu zake na Faustine kwenda kumsalimia ndugu yao kwani mara zote waliondolewa kwa maneno na matusi ya hapa na pale, hatimae Hata vyumba vya kulala kila mtu akawa analala chumba chake wakati huo tayari Debora alikuwa na ujauzito wa Faustine, japo alijaribu kuutoa mara nyingi lakini ilishindikana na hatimae Akaamua kusubiri kujifungua huku kazi zote za ndani zikigeuka kuwa za Faustine,,, miezi tisa ilifika hatimae Debora akajifungua mtoto wa ambaye alikuwa na matatizo ya mdomo kwani ulikuwa upande huku miguu ikiwa haina nguvu, ni wazi alikuwa mlemavu,, Debora aliöna kama ni laana kubwa sana kwake, "Baada ya miezi miwili kupita tangu debora ajifungue, vituko vilizidi sana kwa Faustine, Akiwa amelala alijikuta akiota ndoto ya kutisha iliyomfanya kukurupuka usingizini na kutoka chumbani kwake, alipofika sebuleni alisikia kelele za mahaba chumbani kwa Debora, huku akishangaa kuona mtoto akiwa amelazwa kwenye sofa bila hata kufunikwa nguo yoyote, Faustine alimsogelea mtoto wake na kumbeba vizuri huku akirudi chumbani kwake na kuchukua shuka lake na kumfunika mtoto kisha akarudi na kukaa kwenye sofa, baada ya muda alimuona Debora akiwa amemshika mwanaume mmoja aliyekuwa na tumbo kubwa wakienda kuoga, "Unawaona wanaume sasa,, wee utaendelea kukaa hum na kulea kitoto chako hicho kilemavu, tena najuta kuzaa na wewe maana nadhani ndo sababu ya mimi kuzaa mtoto mlemavu,, na siku siyo nyingi nitamuua" "Alizungumza Debora maneno yaliyomtoa Faustine machozi, akufukuzae hakwambii toka, Faustine alirudi chumbani kwake na kubeba baadhi ya nguo zake kisha akamuweka mtoto vizuri mkononi huyoo akaanza kutoka, alishangaa alipofka mlangoni kuona akisukumwa nusu amdondoshe mtoto,, "TENA UMEJIONGEZA, UNAIONA HII SUMU, NILIKUWA NAWAUWA WEWE NA MWANAO" #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Dar es Salaam, Tanzania

Siku moja nilitupa jiwe na kwa bahati mbaya likampiga bata mzinga na akafa palepale. Japokuwa nilikuwa peke yangu lkn ghafla nilimwona dada yangu nyuma yangu akinitazama. Na akaniambia nimpe elfu moja ili asimwambie mama, nikamwambia sina ila tafadhali usimwambie mama. Siku iliyofuata mama alimwambia dada aoshe vyombo na kusafisha mazingira. Lakini dada akamwambia mama msafiri amesema atafanya, dada akaja na kuniambia nifanye zile kazi la sivyo atamwambia mama nilimuua bata mzinga. Pasipo kulaumu nikazifanya. Siku iliyofuata mama akamwita tena dada na kumwambia akachote maji na kujaza pipa. Dada akamwambia tena mama nimesema nitafanya, akaja kwangu akaniuliza unakumbuka ulimuua bata mzinga? Sasa jaza maji kwenye pipa kama hutaki nimwambie mama. Ikanipasa nikachote maji nijaze pipa. Siku hyo hyo jioni mama akamtuma sokoni kununua nafaka na azisage. Akamamwambia tena msafiri amesema ataenda, akaja kwangu akasema "kumbuka kwamba bata mzinga bado amekufa" nenda sokoni ukanunue mfuko wa nafaka kisha ukasage, kama hutaki basi nitamwambia mama. Nilisimama nikaenda kwa mama huku nikitiririka machozi machoni na nilimkuta amekaa ndani, nikapiga magoti na kumwambia huku nikilia.. "Mama nisamehe tafadhali nisamehe mno. Mm ndio nilimuua bata mzinga kwa bahati mbaya, tafadhali mama nisamehe. Mama akajibu- "Mwanangu siku ile ulipomuua bata mzinga nilikuwa dirishani na nilitazama kila kitu kilichotokea. Dada yako amekufanya mtumwa kwasababu hukutaka kuja kwangu kukiri na kuomba msamaha. Sasa umefanya hv uko huru na dada yako hawezi kukutumia tena. FUNZO, Kila mara tukiwa tunatenda dhambi Mungu anatuona, na dhambi hakika hutufanya kuwa watumwa siku zote. Hivyo tukienda mbele zake tukikiri na kuomba msamaha yeye ni mwingi wa rehema na atatusamehe. *MUNGU ATUSAMEHE DHAMBI ZETU NA ATUWEKE HURU... AMIIN* #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Dar es Salaam, Tanzania

MAPIGO YA MOYO 34 “Salim, Salma… majina na hata mlivyo mmeendana pia. Hongera Salma.” Aliongea Frank na wote wakafurahi. “ila nina ombi kwako Salim. Nakuomba uwe mwaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Salma. Huyu ni zaidi ya mke umepata. Ni zaidi ya mshauri pia ni zaidi wanawake bora ambao ulishawahi kukutana nao. Nitaumia sana nikisikia chochote kibaya kikitokea kwa huyu dada na wewe ndio ukawa msababishaji…. Ni hilo tu. Zaidi ya hayo nawatakia maisha mema na mungu awajaalie kizazi chema.” Aliongea Frank kwa uchungu moyoni lakini akiwa na tabasamu la plasitiki usoni. Wote walicheka na Salim alimyamyuka na kumpa mkono Frank. “nimekulewa. Nakuahidi kumpenda mpaka pumzi yangu ya mwisho wa uhai wangu.” Aliongea Salim na wote wakacheka. *********************** MWISHO************************* Natumaini mmepata elimu ndani ya burudani kutoka kwenye riway a yetu hii yenye hisia kali za mapenzi. Tujifunze kuridhika na wapenzi tulionao kwakua hujui kuwa umpendaye anaweza kubadilika baada ya kuchoka na visa vyako. Hakuna mwalimu wa mapenzi, kila mtu anajua na bwege wa mapenzi akierevuka humshinda professor na kumfanya kuwa matatani. Nyakati za kuumizana mioyo zimeshapita kama kweli utampata yule akupendaye. Maana kupenda sio kazi. Kazi ni unayempenda naye kukupenda kama unanyompenda wewe.. Kwa maoni, ushuri, na kama kuna mtu nimemkwaza kwa namna moja au nyingine, namuomba radhi na awe huru kuniambia kupitia in box na mimi nitajirekebisha. Maana na mimi ni binaadamu na kukosea nimeumbiwa. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Dar es Salaam, Tanzania

MAPIGO YA MOYO 32 Macho ya Frank yalimuangalia na kujilaumu moyoni kumtesa msichana mzuri kama huyo. “pole Frank.” Aliongea Lulu baada ya kumuona Frank akimuangalia. “ahsante, nimeshapoa baada ya kukuona tu.” Aliongea Frank na mama yake akaamua kuondoka kwakua alijua kuwa maongezi yanayoendelea yalikuwa hayamuhusu. “jamani nini tena kimekupata?” aliongea Lulu na kuonyesha ishara za kujali. “ni mitihani tu ya dunia .” aliongea Frank na kumuangalia Lulu kwa macho ya haya. “pole, mungu atakujaalia tu utapona.” Aliongea Lulu kwa hali ya kumuonea huruma Frank. “Lulu, najua kuwa kwa sasa unaweza kuwaza kwa nini nimeamua kukuita. Kusema ukweli, yule msichana niliyekuambia kuwa ni chaguo la moyo wangu. Ndio aliyenisababishia yote haya. Nilipotea njia. Ila kwakua yameshanikuta makuu ndio namekukubuka na kuona thamani yako ikiwa juu ya maisha yangu yaliyobakia. Ni wazi kuwa nakupenda ingawaje nilihisi utakuwa unanibana na kutokuwa huru kuwa na wasichana wengine. Ila nakuapia kuwa hivi sasa najutia kwa kila nilichokutendea na naomba uupokee moyo wangu mkosefu mbele yako wewe uliyejaa uvumilivu na mapenzi ya kweli juu yangu. Nakutamkia kauli kutoka moyoni kuwa nahitaji msamaha wako ili niwe wako kwa mara nyingine.” Aliongea Frank maneno hayo huku machozi yakimtoka na kumfanya Lulu mwenye machozi ya karibu kuanza kulia na yeye. “Frank hakuna mwanaume duniani niliyeiweka rehani roho yangu kwake kama wewe. Ulinifunba macho na kuwa sioni kwa penzi lako. Ni wewe ndiye uliyenifundisha na kunionjesha matamu ya mapenzi. Na ni wewe pia ndio uliyeniingiza kwenye dimbwi la wanaolilia mapenzi na kuniumiza moyo zaidi ya nilivyoumia siku waliyokufa wazazi wangu. Kwanini Frank uliamua kunitenda?? Kwanini uliamua kuninyanyasa kwa maneno yaliyonifanya nitamani kuupoteza uhai wangu??? Kwanini ulinitamkia kuwa mimi si chaguo lako?? Kwanini Frenk??” Aliongea Lulu maneno hayo kwa uchungu na kumfanya machozi yaliashiria uchungu uliopo moyoni mwake kumwagika kama maji. Hali hiyo nayo ilizidi kumuumizi Frank na kumfanya nae azidi kulia kwa uchungu. Kila akisemacho Lulu kilikua cha ukweli. “naomba unisamehe Lulu. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Dar es Salaam, Tanzania

MAPIGO YA MOYO 31 Wiki tatu baadae, Frank alipata fahamu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wazazi wake kumshukuru mungu kwa kumuamsha tena mtoto wao na kumpa uhai. Frank akiwa kitandani. Alikumbuka mbali sana toka anaanza mapenzi. Alikumbuka idadi ya wasichana waliokuwa wakilia na kumpigia magoti bila kosa lolote kumfanyia. Hakuamini kuwa mapenzi hayo hayo ambaye yeye alishayapatia yangewaza kumchenjia na kutaka kumpotezea uhai. Roho ilimuuma sana baada ya kumkumbuka Lulu. Hapo aliamini kuwa huyo ndio alikuwa chaguo lake ambalo mungu amemuandikia. Aliamini kile kilichomtokea ni adhabu kutoka kwa mungu kwa kumkataa mwanamke aliyekuwa na ndoto za kuishi naye bila kuhitaji kitu chochote kwake. Kuna wakati alikua anaamini kuwa toka aanze mapenzi, hakuna msichanana ambaye alikua na malengo naye kama Lulu. Mbali na kumtukana na kumdhalilisha, bado alikua anamuhitaji hata kwakua spare tyre. Taratibu moyo uliokufa ulianza kurudisha matumaini baada ya picha ya Lulu kuganda ubongoni. “mama , naomba muite Lulu aje kuniona.” Aliongea Frank baada ya mama yake kuletea chakula cha mchana. “halafu sijamuona siku nyingi sana huyo msichana na hata nyumbani haji kuni salimia kama zamani. Nitamuonea wapi mimi?” aliongea mama yake Frank kwa sauti ya utaratibu. “ni muhimu sana mama, nenda hata kwao.” Aliongea Frank na mama yake akakubali kufanya hivyo. Saa moja usiku, mama yake Frank aliwasili hospitali akiwa ameongozana na Lulu. Walifika mpaka kwenye kitanda cha Frank ambaye alikuwa amelala muda huo. Lulu alishangaa kumuona Frank akiwa na bandeji mwili mzima. Ilikuwa si rahisi kumtambua kwa haraka kwa jinsi alivyoviringishwa bandeji hio mpaka usoni na kuacha mdomo, Pua na macho tu. Mama yake Frank alimuamsha taratibu Frank. Alipoamka, alistaajabu Frank kumuona Lulu akiwa analengwa lengwa na machozi baada ya kumuona. Kingine kilichomshangaza ni jinsi Lulu alivyo vaa. Alikua kavaa nguo ndefu na kutupia ushungi aliojitanda vizuri. Muonekana wake ulizidi kuwa mzuri. Alikuwa kanenepa kiasi na kufanya Shape yake kuongezeka na kuwa bomba zaidi. #storynzuriiplanet_com

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

Dar es Salaam, Tanzania

MAPIGO YA MOYO 30 Bila kuchelewa, wale wengine walianza kumpa kipigo cha haja Frank kwa magongo waliyonayo na wengine kumcharanga sehemu kadhaa na mapanga. Dakika mbili tu zilitosha kumuacha Frank akiwa hoi pale chini. “ukome kufuata wake za watu.” Aliongea yule mwarabu na kuondoka na kundi lake huku Neila akiwa amemlalia asishuhudie tukio alilofanyiwa Frank. Kipigo walichompa Frank kilimfanya apoteze fahamu. Aliokotwa na wasamaria wema waliokuwa wakipita eneo hilo na kumpeleka hospitali. Taarifa za kuumizwa kwa mtoto wao wa pekee ziliwafikia wazazi wa Frank na kwenda mbio hospitali waliyoelekezwa kuwa Frank yupo. “vipi hali yake Dokta.” Aliuliza mama yake Frank baada ya kumuona daktari aliyekuwa ana muhudumia Frank. “hali sio nzuri sana. Kwakua amepigwa sana maeneo ya kichwani, ndio sababu itakayomfanya kuchelewa kupata fahamu.” Aliongea daktari na kuwaangalia wazazi wa Frank walioonyesha kuchanganyikiwa. “sasa baba unatusaidiaje?” aliongea mama yake Frank kinyonge “kina kipimo cha bodymass index ndio tunachoenda kumpima muda huu ili tujue mwili wake mzima umepata majeraha kiasi gani.” Aliongea Daktari na kuingia kwenye chumba alichotaka kuingia awali. Wazazi wa Frank walirudi kwenye benchi kusibiri majibu ya kipimo hicho. “mwanangu sijui kama atapona.” Aliongea mama yake Frank na kuanza kulia. “mmh mke wangu. Unajichulia ukifanya hivyo. Chamsingi ni kumuombea dua apone na kuwa mzima kama zamani.” Aliongea baba yake Frank na kumbembelea mkewe. Masaa manne baadae, Daktari aliwaita na kuwapa majibu wazazi wa Frank. “majibu yanasema kuwa amevunjika mbavu mbili za kushoto kutokana na kupigwa na kitu au vitu vizito. Kubwa zaidi ni kuwa damu imevuja kwenye fuvu lake la kichwa. Cha kuchukuru mungu ni kwamba damu hiyo haijachanganyika na ubongo. Maana ingekuwa hivyo tungekuwa tunaongelea habari nyingine hapa. Nimewaita ili msaini kama mnakubali mtoto wenu afanyiwe operation kubwa ya kichwa ili tunusuru maisha yake.” Aliongea Daktari na kumfanya mama yake Frank kuanza kulia. Baba yake Frank aliamua kuanguka saini yake na Frank akapelekwa kwenye chumba maalumu cha kufanyia upasuaji. #storynzuriiplanet_com

English Turkish