ImgWonders
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea hashtag

Posts attached with hashtag: #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

SEHEMU 19..... kesho yake ndipo tukakuleta huku katika wodi ya wagonjwa mahututi na hapo kwakuwa mapigo yako ya moyo yalikuwa chini tulijaribu kuyastua ambapo yalipanda kidogo na hapo ndipo tulipokuwekea mashine hiyo ya kupumulia ambayo tumekutolea muda sio mrefu, na ulidumu katika hali hiyo ya kupoteza fahamu huku ukiwa unapumulia mashine kwa muda usiopungua takribani wiki nne kasoro mpaka siku hii ya leo ambayo ndo umepata fahamu” dokta hashimu alimaliza maelezo yake aliyoyatoa kwa kirefu ambapo Mr alex alimuelewa vema… “Na vipi kuhusu gharama na huduma ambazo mlikuwa mnanipatia, ni nani ambae alikua anashughulika na hili?” Mr alex aliuliza tena kwani alizijua vyema hospitali za bongo, huwezi kutibiwa kama utakuwa huna pesa… “Usijali gharama zote nilizitoa mimi mpaka kufikia leo hii, nah ii nimeifanya kwa moyo kwani nilipatwa na huruma sana baada ya kuona mwili wako ukiwa katika hali mbaya, hapo nimuomba Mungu anisaidie niweze kupambana kufa na kupona kuhakikisha kwamba unarudi katika hali yako ya kawaida, na ninamshukuru Mungu kwa kutenda muujiza mpaka wewe unapumua kwa wakati huu” alizungumza dokta hashim. Mr alex alipigwa na butwaa baada ya kusikia kua dokta hashimu alisimamia gharama zote za yeye kutibiwa kwani hakuamini kama katika dunia hii bado kulikua na watu wenye moyo kama dokta hashimu, hii ni kutokana na kuona jinsi dunia inavyoenda, watu hawasaidiani, watu wanachukiana, watu wanadharauliana, watu wanauana, wenye pesa wanawadharau masikini kwa kuwaona hawapaswi kuishi, sasa alishangaa kuona mtu mwenye moyo kama ule kuwepo katika kizazi hiki cha nyoka… “Nashukuru sana dokta Mungu akubariki na akuzidishie kipato chako kaka yangu” Mr alex alijikuta akizungumza maneno hayo huku machozi yakimtoka, hakika alijiona ni mwenye bahati sana, ingawa alikua ana fedha za kutosha kama pasinge tokea mtu ambae angejitolea kumsimamia mpaka hapo alipofikia, angeshakua marehemu kwani pesa alikuwa nazo sawa lakini nani akijua kwamba pesa za kujilipia matibabu alikuwa nazo ilihali yeye alikuwa kapoteza fahamu kwa muda wa miezi miwili? #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

SEHEMU 18..... Niligeuka upande ule ambao ulikuwa na jopo la madaktari, niliwaangalia kwa awamu na hapo niliwauliza nipo wapi maana chumba ambacho nilikuwepo mara ya kwanza kilikua ni tofauti na chumba ambacho nilikuwepo kwa muda huo… “Tulia Mr alex kwanza pole kwa yaliyokukuta” alizungumza mmoja wa madaktari ambaye alionekana ndiye mkubwa wa jopo lile la madaktari waliokuwepo mule ndani, muda huo nilikuwa najiuliza maswali mengi sana kichwani, kwanza nilijiuliza wamejuaje jina langu na nipokumbuka kwamba nilikuwa na vitambulisho pamoja na vyeti vyangu basi nilijikuta mawazo hayo yakiisha na hapo ndipo nilipokumbuka kuwa kuna dokta alikua ananiondelesha, basi nilianza kumjibu yule dokta maswali ambayo alikua akiniuliza… “Pole sana Mr alex kwa yaliyokukuta” alizungumza daktari yule ambae alikua akizungumza kwa umakini wa hali ya juu.. “Nashukuru sana dokta…” “Sawa naitwa dokta Hashim, wenzangu hapo ni dokta jack, dokta john,dokta abdul na dokta Razaq” alitambulisha dokta hashimu na baada ya hapo aliendelea.. “Mimi nahusika na masuala ya mwili kwa ujumla lakini nimebobea katika kutibu magonjwa ya moyo, ini pamoja na figo, huyo dokta jack yeye amebobea katika maswala ya mifupa, dokta abdul yeye amebobea katika maswala ya ubongo na mshtuko na dokta razaq yeye amebobea katika maswala ya psychology(saikolojia) pamoja na maswala ya kizazi(reproductive issues as general)” dokta hashimu aliweka nukta na kumeza funda la mate kabla hajaendelea… “Nashukuru kwa utambulisho dokta, samahani kwa swali hili ambalo nataka kukuuliza” aliongea Mr alex “Bila samahani, unavyotuona hapa tupo kwaajili ya kukujibu maswali ambayo yatakuwa yanakutatiza” alijibu dokta hashim na kumtoa wasiwasi Mr alex “Tangu nimeletwa hapa nina mda gani?” Mr alex aliuliza “Ulifikishwa hapa muhimbili miezi miwili iliyopita, lakini mwezi mmoja kabla ya kuingizwa katika chumba hiki cha wagonjwa mahututi(ICU) ulipata fahamu lakini manesi ambao walikua zamu siku hiyo wanasema ulivyopata fahamu ulipiga ukulele na baada ya hapo ulipoteza tena fahamu, kesho yake ndipo tukakuleta huku katika wodi ya wagonjwa mahututi na hapo kwakuwa mapigo yako ya moyo yalikuwa chini ... #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

SEHEMU 17. kitendo cha ghafla tuu na kutahamaki tayari nikawa nimelifikia bamsi lile, nilijaribu kufunga breki za ghafla lakini breki zilifeli, hapo nikalivaa bamsi lile ambapo tax ile niliyokua naendesha wakati huo tukiwa wawili tuu kwenye tax ile, tax ile irushwa juu na baada ya kutua iliviringika mara tano mfululizo, yule dereva tax nilokuwa nipo nae nilishuhudia akikata roho wakati bado hatujatolewa katika gari ile na baada ya kushuhudia tukio la kukata roho kwa yule dereva tax sikujua tena kilichoendelea kwani nilipoteza fahamu” alizungumza Mr alex huku machozi yakimtoka, alitoa handkerchief(hengachifu/ leso) yake katika moja ya mfuko wa koti la suti ambalo alikua amelivaa na kujifuta machozi… “Daaa aise pole sana baba kwa yaliyokukuta” alizungumza michael katika hali ya huzuni kubwa na kuumia moyoni “Nashukuru mwanangu nimeshapoa” alijibu Mr alex “Enhe baada ya hapo ikawaje baba” aliuliza tena michael na kufanya Mr alex kuendelea kusimulia kilichomkuta baada ya ajali ile mbaya kuwahi kutokea katika maisha yake.. “Basi nilipokuja kupata fahamu nilijikuta nipo hospitalini ambapo nilikuja kugundua kuwa ilikua ni hospitali ya taifa ya muhimbili baada ya kuwauliza wahudumu ambao walikua wakipishana kuingia katika chumba ambacho nilikua nimelazwa, nilijaribu kuamka na hapo nilikumbana na maumivu makali sana ambayo yalinifanya nitoe ukulele hafifu na baada ya hapo nilipoteza tena fahamu, siku ambayo nilikuja kupata fahamu nilisikia mchakacho wa kama mtu akikimbia na baada ya hapo nikisikia sauti ya ikisema kwa nguvu.. “Doktaa ameamkaaa” Hazikupita hata sekunde tano liliingia jopo la madaktari wapatao watano ambapo walipoingia walitabasamu baada ya kuona nimefungua macho, hapo nilitolewa mashine ya (Oxygen) oksijeni ambayo nafikiri ndiyo iliyokua ikinisaidia kupumua kipindi ambacho nilikua nimepoteza fahamu, baada ya mashine ile kutolewa ndipo nilipoanza kuangaza macho huku na huko, nilijaribu kuvuta kumbukumbu jinsi ilivyokua na hapo niljikuta machozi yakinitoka baada ya kukumbuka matukio yote niliyokutana nayo ambayo yalipelekea mimi kuwa hapo hospitali ya taifa ya muhimbili kwa kipindi hicho, #ITAENDELEA

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photo
vennita_mwita

Vennita Mwita

@vennita_mwita ....Niliondoka nduki hadi hospitalini kumuona bibi yangu, sikujali kubadili nguo. Nilikuta yuko vile vile tuu, hajaongea. Nilipatwa huzuni kidogo tena ila nilijionesha kama jasiri ili dada Monica asipatwe na wasiwasi. Jioni yeye alirudi parokiani na Padri, mimi nikalala tena wodini. Nilihisi uchovu kwa kuwa nilitumia muda mwingi kujiandaa na mtihani, hivyo usiku huu mapema tuu nilisinzia. Nilisogeza kiti, nikalaza kichwa changu kwenye kitanda cha bibi, kama kawaida, nikalala. Sikumbuki hata niliota vitu gani yaani, ila niliota vindoto vingi vingi tuu. Nikiwa katika hivyo vindoto vyangu, nilistushwa na mkono wa bibi kichwani kwangu, niliamka, tulitazamani tuu, ni kama alitaka kuongea ila hakuweza, nilimuita nesi, nae akamuita dokta, wakafanya yao, wakaniambia atakuwa sawa, waliinua kitanda kidogo upande wa kichwani kwake, akawa kama kanyanyuka kidogo, wakaondoka. Baada ya muda bibi alilala, nami nikalala pia. Nikaota tena vindoto vyangu, vilinisumbua, nikawa nastuka stuka tuu usingizini. Lakini sivikumbuki sana.. Nilistuka asubuhi nikiwa mchovu mchovu tuu. “Aisee! Kaka za siku? Fungate limeisha? Sikutaka kukusumbua kaka, ndio maana nilikuwa kimya, ila hali ya bibi ndio kama hii. Sasa anajua ukweli woote!’ nilijikuta nikiongea tuu baada ya kumuona kaka pale wodini, maana tangu tuanchane siku ya harusi nilikuwa sijaongea nae kabisaaa! Niliona kama kabadilika, kawa mkubwa. Sijui kwa kuwa hatukuonana kwa wiki nzima ama la! Kumbe alinitafuta sana kwa simu, na aliponikosa aliwasiliana na Padri na akamwambia ninayopitia! ‘Pole Paul, nilidhani utanisubiri tuongee na bibi pamoja, lakini hata sasa ni vyema, tumuombee tuu apone. Padri kaniambia umekuwa ukilala na kushinda hapa, sasa waweza kwenda kupumzika kidogo, nami nikae na bibi, kama hutojali!’ kaka alisema. Nilikataa, ni kwamba sikuwa tayari kumuacha bibi yangu peke yake. Kaka aliniambia hajaongea na mke wake (binamu) kuhusu mimi, alitaka nifanye mimi mwenyewe nikiwa tayari......! #Itaendelea

PUTENGA OG (@putenga_og) Instagram Profile Photo
putenga_og

PUTENGA OG

@PUTENGA_OG NJIA 14 ZA KUONDOA TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI Kati ya matatizo makubwa kabisa yanayowasumbuwa wanaume katika suala la kujamiiana ni kufika kileleni mapema. Takwimu zisizo rasmi zinasema kuwa, wanaume 7 kati ya 10 wanapatwa na tatizo hii. Malalamiko yanayotolewa na baadhi ya wanaume yanathibitisha kwamba, muda wa kumaliza tendo huwa kati ya nusu dakika na dakika mbili kwa tendo la kwanza, huku wengine wakimaliza hamu katika hatua za awali tu wakati wakiandaana na kukosa hamu kabisa ya tendo la ndoa. Hata hivyo wale wanaoweza kusimama tena mara baada ya tendo la kwanza wanakiri kuchelewa kidogo, ingawa bado suala la kutangulia kufika kileleni kabla ya mwanamke limekuwa likiwahuzunisha wanaume wengi wa rika zote vijana hata wazee. Ndoa nyingi zimevunjika chanzo kikiwa ni tatizo hili. Karibu kila pembe ya dunia kunasikika vilio toka kwa wanaume wakilalamika kukabiliwa na tatizo la kuwahi kufika kileleni, ambalo limewafanya waonekane si lolote kwa wenzi wao. Ni ukweli usio pingika kuwa mwanaume anapowahi kufika kileleni kabla ya mwenzake humwacha mwanamke na huzuni kwani anakuwa hajapata kile anakihitaji katika tendo hilo. Katika kujitibu tatizo hili jambo la kwanza ni kuelewa ni nini kimesababisha tatizo hilo kwa upande wako. Njia 14 za kujitibu tatizo la kuwahi kufika kileleni: 1. Acha mawazo Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe. Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!. 2. Jitibu magonjwa yafuatayo Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli. ....#Itaendelea

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photo
vennita_mwita

Vennita Mwita

@vennita_mwita Akasema kwa kuwa polisi wanaelewa stori yote, basi nisiwe na shida na yeye pia hana wasiwasi kumuacha bibi mikononi mwetu. Akaondoka. Baadae dada Monica na Padri Mollel walifika wakiwa na chai, nilikunywa, Padri alipewa taarifa na dokta usiku uleule kuwa bibi kazinduka, hivyo alikuja akiwa na taarifa. Hadi sasa bibi alikuwa hajaongea neno lolote, alikuwa akitazama tuu. Nasi hatukumuongelesha, tulitii masharti ya dokta. Lo! Bibi jamani, alikuwa kama mtoto pale kitandani. Nilishinda pale pale hospitali tena,niliamini bibi atapona kwa kuwa sasa alikuwa na fahamu, japo hakuongea. Kuna watu ni kama malaika, maana tangu nikutane na bibi, sikukumbuka tena kuhusu Dulla kule Mbeya, na hata sikutuma ada yake. Duuh! Moyo uliniuma, sikutaka anione kama tapeli. Na sasa sikuwa na simu yangu, ilipasa nisubiri kaka atoke fungate ndio nimuombe namba! Kumbe bwana Padri alishafanya kila kitu akanitunzia tuu risiti za benki ili nimrejeshee pesa yake baadae. Na Dulla sasa alikuwa shule, nilifurahi sana. Padri ndie alikuwa na simu yangu, aliitunza maana kweli sikuwa na muda nayo kabisa, na yamkini ningeipoteza! Alinisihi nirudi nyumbani nikajiandae na mtihani wangu wa mwisho wa udereva kule VETA. Mmmmh nimuache bibi hapa kweli!? ‘Padri, alama za barabarani zoote nazifahamu,nadhani nitajikumbushia hapa hapa hospitalini na pia mtihani kwa vitendo sio shida kwa kuwa naweza kuendesha gari, hospitalini, mahakamani, vituo vya polisi, ikulu na ofisi za serikali, mbuga za wanyama, gerezani n.k ni maeneo yasiyoruhusiwa kupiga honi, kwa hiyo siwezi kufeli kesho, naomba tuu nikae na bibi yangu kwa muda zaidi hadi atakapo ongea tena!’ nilimwambia Padri. Alikubali. Mapema asubuhi nilienda nyumbani, nikavaa sare za chuo, tayati kwa mtihani. Dada Monica alibaki na bibi wodini, Padri aliekuwa parokiani kwa majukumu yake. Nilifanya mtihani vyema tuu, haukuwa mgumu, nilimjulisha mwalimu kuwa nina mgonjwa hospitali, ili anipange wa mwanzoni mwanzoni kuendesha gari (practical). Mida ya saa nane nilikuwa tayari mhitimu wa mafunzo ya udereva kwa gari za abiria! Ndoto yangu ilitimia! Nilikuwa na hakika ya kufaulu! #Itaendelea leo

Vennita Mwita (@vennita_mwita) Instagram Profile Photo
vennita_mwita

Vennita Mwita

@vennita_mwita ..Nililala hospitali na bibi yangu, hadi asubuhi alikuwa hajapata fahamu. Mtihani wangu ulikuwa ukikaribia (mafunzo ya udereva VETA). Sikujua cha kufanya, nilisahau kuhusu Dulla kule Mbeya. Nilikuwa mtu aliechanganyikiwa. Sikujua hata simu yangu ilipo. Sikutaka kutoka hospitalini pia. Bibi yangu alikuwa kalala vile vile. Nilikumbuka mama yangu alivyokufa na nikashinda na kulala nae bila kujua kama kafa. Sikutaka iwe hivi kwa bibi yangu pia. Nilianza kumuongelesha, nilimsimulia jisi gani nampenda, jinsi nitaishi nae. Nilimwambia mimi ni zawadi yake toka kwa Eliza wake. Nilimsimulia jinsi ntamtembeza jijini akipona. Basi nilikuwa nikiongea mambo mbali mbali kwa sauti peke yangu, nikiamini bibi anasikia pia japo hanijibu. Ilifika jioni hali ikiwa vile vile tuu. Nilihofu. Kwa muda wote sikumuona mjomba wala ndugu zake pale hospitali, sikuwa na simu ili nimpigie kaka mwalimu pia. Usiku tulikula, nikaoga mle mle wodini kwa bibi, wenzangu wakarudi parokiani, mimi nikalala hospitali. Sikutaka kuwa mbali,nilisogeza kiti tena, nikalaza kichwa changu kitandani kwake. Nikajiongelesha mwenyewe kwa muda mrefuu, nikapitiwa usingizi hapo hapo. Nilistushwa na mkono wa mtu kichwani kwangu, nikaamka, alikuwa bibi yangu! Bibi alizinduka, akanishika kichwani! Nilifurahi nikaita tuu bibi yangu jamani, hakunijibu, alinitazama tuu, alikuwa kawekwa kitu mdomoni hivyo hakuweza kuongea, nilifungua mlango nikamuitaka nesi kwa nguvu, sikutaka kutoka kwenda mbali maana sikutaka kumuacha bibi peke yake yamkini akapoteza fahamu tena. Nesi alifika akamtazama na kisha akaenda kumuita dokta. Walimfanyia huduma na vipimo, wakamuwekea dripu tena. Wakamtoa mashine/chuma cha mdomoni wakasema nimuache apumzike, nisimuongeleshe, wakatoka. Nilikaa pale pale, tukitazamana tuu, baada ya muda alilala usingizi, nilimtazama kama anapumua, sikulala hadi asubuhi. Asubuhi na mapema Paroko wa Ileje alifika, akasali akambariki bibi, akaniaga, akasema kwa kuwa bibi yuko vizuri sasa, basi yeye anasafiri kurudi Mbeya kuendelea na kazi, akaahidi kuendelea kuwasiliana nasi.. #Itaendelea leo

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

SEHEMU YA 16 “Wakati nikiwa katika hali hiyo ya bumbuwazi nilipatwa na mshtuko baada ya kuona viumbe wale wakizidi kuongezeka kila baada ya sekunde kadhaa, ni kama vile mshtuko ule ulinigutua katika bumbuwazi lile na hapo ndipo nilipo usikia vyema ukulele wa yule dereva tax akiniita kwa nguvu kuwa nirudi kwenye gari ili tuweze kuondoka kwa eneo lile halikua salama kuendelea kubaki, ilifika muda yule dereva tax akashuka katika gari ili aje anivute tuingie kwenye gari, hapo niligeuka haraka baada ya kusikia ukulele mkubwa ambao aliutoa yule dereva tax kuonesha kwamba alikua katika hatari kubwa, na kweli nilipogeuka niliona chatu mwingine mkubwa kiasi akiwa anaanza kujiviringisha katika mwili wa dereva tax yule ambae alikua akipiga makelele ya uoga ili aweze kummeza, hapo nilitoka mbio mbio mpaka eneo alilokuwepo yule chatu ambae alikua anajiviringisha katika mwili wa dereva tax, hapo niliitoa pistol(bastola) yangu kisha nikaikoki vyema na kilichofuata nilisambaratisha kichwa cha yule chatu ambae alikua akijiandaa kummeza yule dereva tax, hapo nilimsaidia kujitoa kwa chatu yule ambae tayari alikua ameshapoteza uhai wake na kwakua yule dereva tax hakuwa sawa nimsaidia kumuingiza kwenye gari, hapo nilikaa sehemu ya usukani na kuliondoa gari kwa kasi ya ajabu kwani wale chatu wengine walikua wakija kwa kasi eneo lile ambalo tulikuwepo kwa lengo la kutudhuru, kutokana na mwendokasi ambao nilikua nikiutumia niliweza kufika mtwara mjini kwa kutumia dakika kumi tuu,spidi niliyoingia nayo katika barabara ya lami kila mtu aliyekuwepo barabarani aliweka mikono kichwani na wengi walitabiri kwamba tutapata ajali kwa mwendo ule, wengine walidhani kuwa huenda sisi ni majambazi tumetoka kupora mahali… Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo basi laja, kama jinsi watu walivyotabiri kuwa tutapata ajali ndivyo ilivyokua, kipindi nakanyaga mafuta mpaka mwisho sikuweza kugundua kuwa mbele palikua na bamsi nah ii ni kutokana na kutokujua vyema barabara ile, ni kitendo cha ghafla tuu na kutahamaki tayari nikawa nimelifikia bamsi lile, nilijaribu kufunga breki za ghafla lakini breki zilifeli.. #ITAENDELEA

English Turkish