ImgWonders
  1. Homepage
  2. @storynzuriiplanet
  3. 1847775195719245136
Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo

storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

🔵East African Artist 🔥Mr Romantic TANZANIANBOY🇹🇿 YouTube Channel.. 👇👇👇👇👇

https://youtu.be/I_A4hfigsMw

+255 659777713

shebyzdayo12@gmail.com

dar es salaam Dar es Salaam, Tanzania

MAPIGO YA MOYO 31 Wiki tatu baadae, Frank alipata fahamu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wazazi wake kumshukuru mungu k - 1847775195719245136

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photo
storynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "MAPIGO YA MOYO 31

Wiki tatu baadae, Frank alipata fahamu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wazazi wake kumshukuru mungu k" at Dar es Salaam, Tanzania - 1847775195719245136
Dar es Salaam, Tanzania

MAPIGO YA MOYO 31 Wiki tatu baadae, Frank alipata fahamu kwa mara ya kwanza na kuwafanya wazazi wake kumshukuru mungu kwa kumuamsha tena mtoto wao na kumpa uhai. Frank akiwa kitandani. Alikumbuka mbali sana toka anaanza mapenzi. Alikumbuka idadi ya wasichana waliokuwa wakilia na kumpigia magoti bila kosa lolote kumfanyia. Hakuamini kuwa mapenzi hayo hayo ambaye yeye alishayapatia yangewaza kumchenjia na kutaka kumpotezea uhai. Roho ilimuuma sana baada ya kumkumbuka Lulu. Hapo aliamini kuwa huyo ndio alikuwa chaguo lake ambalo mungu amemuandikia. Aliamini kile kilichomtokea ni adhabu kutoka kwa mungu kwa kumkataa mwanamke aliyekuwa na ndoto za kuishi naye bila kuhitaji kitu chochote kwake. Kuna wakati alikua anaamini kuwa toka aanze mapenzi, hakuna msichanana ambaye alikua na malengo naye kama Lulu. Mbali na kumtukana na kumdhalilisha, bado alikua anamuhitaji hata kwakua spare tyre. Taratibu moyo uliokufa ulianza kurudisha matumaini baada ya picha ya Lulu kuganda ubongoni. “mama , naomba muite Lulu aje kuniona.” Aliongea Frank baada ya mama yake kuletea chakula cha mchana. “halafu sijamuona siku nyingi sana huyo msichana na hata nyumbani haji kuni salimia kama zamani. Nitamuonea wapi mimi?” aliongea mama yake Frank kwa sauti ya utaratibu. “ni muhimu sana mama, nenda hata kwao.” Aliongea Frank na mama yake akakubali kufanya hivyo. Saa moja usiku, mama yake Frank aliwasili hospitali akiwa ameongozana na Lulu. Walifika mpaka kwenye kitanda cha Frank ambaye alikuwa amelala muda huo. Lulu alishangaa kumuona Frank akiwa na bandeji mwili mzima. Ilikuwa si rahisi kumtambua kwa haraka kwa jinsi alivyoviringishwa bandeji hio mpaka usoni na kuacha mdomo, Pua na macho tu. Mama yake Frank alimuamsha taratibu Frank. Alipoamka, alistaajabu Frank kumuona Lulu akiwa analengwa lengwa na machozi baada ya kumuona. Kingine kilichomshangaza ni jinsi Lulu alivyo vaa. Alikua kavaa nguo ndefu na kutupia ushungi aliojitanda vizuri. Muonekana wake ulizidi kuwa mzuri. Alikuwa kanenepa kiasi na kufanya Shape yake kuongezeka na kuwa bomba zaidi.

Comments

English Turkish